#325
Hapa katika dunia tunaachana
Wokovu
Couplet 1
Hapa katika dunia tunaachana mara nyingi. Lakini kwa Mwokozi wetu, hatutatengwa naye.
Refrain
Baba Mungu awe pamoja nawe. Akulinde katika njia, Uende katika amani, Tu pamoja kwa maombi.
Couplet 2
Tukitengwa na rafiki, tunatumaini kwa Mungu, Yeye atatufariji, kwa Neema na upendo.
Refrain
Baba Mungu awe pamoja nawe. Akulinde katika njia, Uende katika amani, Tu pamoja kwa maombi.
Couplet 3
Adui wetu watatu, mwili, dunia na shetani. Uepuke wote hawa, ngao, neno lake Bwana.
Refrain
Baba Mungu awe pamoja nawe. Akulinde katika njia, Uende katika amani, Tu pamoja kwa maombi.
Couplet 4
Baba Mungu twakuomba, uchunge huyumwana wako. Pamoja na jamaa lake, hata siko ya milele.