#326
Siku kuu ya Mungu imekaribia
Wokovu
Couplet 1
...Siku kuu ya Mungu imekaribia, mwaliko umetumwa kwako. Mda ni mfupi, tujitayarishe, kwenda kumlaki Bwana Yesu.
Refrain
Siku inakuja, yawaka kama Moto, kimbia hukumu yake Bwana. Siku inakuja, yawaka kama Moto, kimbia hukumu yake Bwana.
Couplet 2
Wewe unasema: ni siku nyingi twaalikwa na wahubiri. Ufahamu kama siku moja kwa Bwana, ni kwama miaka elfu moja.
Refrain
Siku inakuja, yawaka kama Moto, kimbia hukumu yake Bwana. Siku inakuja, yawaka kama Moto, kimbia hukumu yake Bwana.
Couplet 3
Rafiki ’jiulize, je umeokoka, kwa matendo na tabia yako? Kama bado, mpendwa, hujui amani, fanya hima uokoke sasa.
Refrain
Siku inakuja, yawaka kama Moto, kimbia hukumu yake Bwana. Siku inakuja, yawaka kama Moto, kimbia hukumu yake Bwana.