#323
Nakutegemea Yesu unilinde hapa
Wokovu
Couplet 1
Nakutegemea Yesu, unilinde hapa chini. Njia yangu ndefu sana wewe ndiwe kiongozi.
Refrain
Unitie nguvu kweli majaribu na mashaka vyazunguka roho yangu. Kweli utaniwezesha.
Couplet 2
Nilikuwa mbali nawe, hata hivyo ’kanifia. Ulipenda roho yangu, nakupenda Bwana wangu.
Refrain
Unitie nguvu kweli majaribu na mashaka vyazunguka roho yangu. Kweli utaniwezesha.
Couplet 3
Kao nzuri la Mbinguni, natamani kufikako. Unitengeneze tena yainue macho yangu.
Refrain
Unitie nguvu kweli majaribu na mashaka vyazunguka roho yangu. Kweli utaniwezesha.
Couplet 4
Hapa chini duniani ibilisi anguruma. Anataka kutumeza, sifa kwako twazunguka.