Indirimbo Zikundwa Open in the app

#322

Nashika njia ya kwenda Mbingu

Wokovu

Couplet 1

Nashika njia ya kwenda Mbingu, mimi msafiri duniani, naishi kwa taabu na mateso mengi. Bali nakaza mwendo nifike Mbingu.

Couplet 2

Ijapo shida zanizunguuka, mimi msafiri njia, nashika njia nifike Mbingu; nitarithi pamoja na Yesu, nitarithi pamoja na Yesu. :/:

Couplet 3

Wenzangu wote wananigombeza na marafiki wananicheka. Nasumbuliwa hata na wanangu, natazama Yesu rafiki Mwema.

Couplet 4

Ninachofanya maishani mwangu, nimpendeze Mungu aliye Mwema. Nijapoteswa, ninatumaini kuingia Mbingu, ni nchi ya raha.