Indirimbo Zikundwa Open in the app

#321

Mwokozi Mzuri ni Yesu Kristo

Wokovu

Couplet 1

Mwokozi Mzuri ni Yesu Kristo, ninamshukuru sana. Alinitafuta kwa njia mbaya, ni mali ya Yesu Mwana.

Refrain

Kwa Damu nafunguliwa, kwa Damu nafunguliwa. Alitoa yote kwa mimi na wote, kwa Damu nafunguliwa.

Couplet 2

Alibeba dhambi Msalabani, alitukomboa sote. Barua za deni na mashitaki, alizipasua zote.

Refrain

Kwa Damu nafunguliwa, kwa Damu nafunguliwa. Alitoa yote kwa mimi na wote, kwa Damu nafunguliwa.

Couplet 3

Ni heri kujua makimbilio, wakati wamajaribu. Nashinda kwa nguvu ya Damu yake, asanti Mtakatifu.

Refrain

Kwa Damu nafunguliwa, kwa Damu nafunguliwa. Alitoa yote kwa mimi na wote, kwa Damu nafunguliwa.

Couplet 4

Aliteswa sana kwa Getsemane, uchungu aliunyweshwa. Lakini kwa mwisho Msalabani, alisema imekwisha.