Indirimbo Zikundwa Open in the app

#319

Nafurahia Wokovu niliopata

Wokovu

Couplet 1

Nafurahia Wokovu niliopata kwa Yesu, nitasifu Mungu wangu daima huko Mbinguni. Wokovu niliopewa, na unanirusha juu, kw’ajili ya shangwe kubwa, inayoimba rohoni.

Couplet 2

Silinganishe Wokovu wangu na kitu kingine. Kwani vyote vinakosa, bei ya Wokovu wangu. Mwokozi alinifia, alinilipia Damu, nayo ni ya bei ghali, safi ya Mwana wa Mungu.

Couplet 3

Ninaupenda Wokovu, wanitosha kwa matata, kwani Bwana wa Wokovu, hakufuata makelele. Aliwaponya wagonjwa, na alifufua wafu, akahubiri injili, alituonyesha njia.

Couplet 4

Ninakusifu Mwokozi, kwani umeniokoa, umenitosha kwa giza, na sasa niko nuruni. Mwenye upendo ni wewe, Neema yake ni kubwa, ulinitosha kabisa, katitka pori na giza.