Indirimbo Zikundwa Open in the app

#318

Nimeliona Pendo kubwa mno

Wokovu· TAMBI Eae Munaongo, 1942

Couplet 1

Nimeliona Pendo kubwa mno, na pendo hilo nalifurahia. Na jina lake mwenye kunipenda, Ni Mungu Baba tena Yesu Mwana. :/: Upendo wako nausifu sana, ewe Mungu nawe Yesu Kristo. :/:

Couplet 2

Mimi mtoto mdogo mbele yako, nakuhitaji unisaidie. Kwa kila kazi na kwa hali zote, kwa majaribu katika dunia. :/: Usiniache mimi peke yangu, uwe nami kwa safari yangu. :/:

Couplet 3

Nikikuomba uje kwangu Yesu, ukija tena ninaona hofu. Utanishika mimi mwanaDamu, sitendi vema mimi mwenye shaka. :/: Nilipendalo silitendi tena, ninafanya nisilolipenda. :/:

Couplet 4

Nilipokuwa mtoto mchanga, na niliwaza mambo ya utoto. Na kwa wakati wakuwa mzima, nilibadili mambo ya utoto. :/: Matumaini na imani yangu, inakwamilishwa kwa injili. :/:

Couplet 5

Nimeliona pendo la Mwokozi, aliyenikomboa kati Damu. Na Damu hiyo si Damu ya nyama, ni Damu yake Bwana Yesu Kristo. :/: Ee! Mwenye haki kwa wasio haki, umetoa maisha na pendo.:/: