Indirimbo Zikundwa Open in the app

#317

Sisi tuliokoka na tunashangilia

Wokovu· Wimbo wa kirundi · TAMBI Eae Munaongo, 1952

Couplet 1

Sisi tuliokoka na tunashangilia, twapita unlimwengu na tuna amani.

Couplet 2

Mwapenda vya dunia mbona hamvishibe, hata wababu zenu hawakuviweza.

Couplet 3

Dunia itaisha na vyote vilivyomo. Nyumba na mashamba, akili na pombe.

Couplet 4

Vinavyowadanganya havitawaokoa, vitakuwa majivu, arudipo Bwana.

Couplet 5

Na wenye roho ngumu, tuwafanyie nini? Mbona tunawaonya na mnakataa?

Couplet 6

Hatuna la kufanya, tutahamia Mbingu. Tunasikitika ju’ ya wenye dhambi.

Couplet 7

Tutakwenda Mbinguni, kuona wateule, vijana ’takatifu waliotakaswa.

Couplet 8

Tutashirikiana na makabila tena, ila waliotubu na kuoshwa na Yesu.