Indirimbo Zikundwa Open in the app

#316

Nyota kubwa inang’aa

Wokovu· TAMBI Eae Munaongo, 1949

Couplet 1

Nyota kubwa inang’aa, inang’aa nguvu sana, ahadi ya zamani. Iling’aa tangu mbele manabii wali’ona, ilingoja wakati. :/: Iling’aa, nyota kubwa yang’aa. :/:

Couplet 2

Manabii waliona nyota ile iling’aa ilikuwa kwa mbali. Na Bwana aliona nyota kutoka Yakobo kwa maono rohoni. :/: Iling’aa, nyota toka Yakobo. :/:

Couplet 3

Mashauri ya Mbinguni yalipokuwa tayari Mwokozi alifika. Nyota yake itang’aa kwa milele na milele, haizimike kamwe. :/: Itang’aa, itang’aa milele. :/:

Couplet 4

Iling’aa, iling’aa, iling’aa, iling’aa, ilikuwa kwa mbali. Ni majusi walipata kuiona mashariki nyota ya Bwana Yesu. :/: Iling’aa, iliangaza wazi. :/:

Couplet 5

Ni Isaya anasema kama mwana tumepewa, Mwokozi azaliwa. Anaitwa Wa ajabu na Mkuu wa amani, watu wake furahi. :/: Wa ajabu, Wa ajabu Masiya. :/:

Couplet 6

Mashariki, Magaribi, Kaskazini na Kusini inaangaza pote. Watu wote wameisha kusikia Neno lake linaangaza wote. :/: Wa ajabu, Wa ajabu Masiya. :/: