Indirimbo Zikundwa Open in the app

#314

Kuomba ni agizo jema mno

Wokovu

Couplet 1

Kuomba ni agizo jema mno, kupata ni ahadi tamu kweli. Likiwa nene nguvu na matata; tazama afungaye kwa upendo.

Refrain

Sifa kwa Mungu Baba wetu, Anawaunga wawili leo, Alicho unganisha Mungu Mwana aDamu asitenganishe.

Couplet 2

Tuombe kwa agizo la Mwokozi, tuliokuwa wenye kupotea, lakini sasa tunaunganishwa kwa jina lake Bwana Yesu Kristo.

Refrain

Sifa kwa Mungu Baba wetu, Anawaunga wawili leo, Alicho unganisha Mungu Mwana aDamu asitenganishe.

Couplet 3

Uwe rafiki yake Bwana Yesu, msiharibu pendo kwa maneno, mkiheshimu Mungu kati yote, amani ya Yesu ’takuwa nanyi.

Refrain

Sifa kwa Mungu Baba wetu, Anawaunga wawili leo, Alicho unganisha Mungu Mwana aDamu asitenganishe.

Couplet 4

Mungu aliumba mme na mke na ikingali hivyo hata leo, na ninyi ndugu mnaunganishwa, katika jina lake Bwana Yesu.

Refrain

Sifa kwa Mungu Baba wetu, Anawaunga wawili leo, Alicho unganisha Mungu Mwana aDamu asitenganishe.

Couplet 5

Salamu hii toka sisi wote, neno la Mungu la kuwafariji. Wakolosai kwa sura ya tatu haya ya kumi na nane inatosha.