#313
Kumbe wakati wapita mbio
Wokovu
Couplet 1
Kumbe wakati wapita mbio, ni sawa jana mlipofika, mlitumika pamoja nasi, na sisi wote tulifurahi.
Couplet 2
Na kazi yenu tuliipenda, hamkuchoka kutufurahisha. Taabu yenu haiko bure, ni Bwana Yesu atawalipa.
Couplet 3
Mnaporudi mlikotoka twaomba Mungu mrudi tena. Kutumika pamoja nasi, kazi ni nyingi zinazowangoja.
Couplet 4
Machozi mengi yalengalenga kwa macho yetu mnapotuacha, ni siku gani tutaonana. Mwenyezi Mungu ndiye ajua.
Couplet 5
Salamu sana kwa nchi yenu, kwa makanisa na Wakristo, sema Mwokozi ni Yesu peke, aliyekwisha kutusamehe.
Couplet 6
Pasha habari ya ile hati ya mashitaki imetundikwa na imekazwa kwa nguvu sana, Msalabani ifedheheke.
Couplet 7
Na ile hati ya adui, ni Bwana Yesu ameifuta, hakuna tena hukumu kwetu tunaokaa ndani ya Yesu.