Indirimbo Zikundwa Open in the app

#312

Zaburi 117: 1-2

Wokovu

Couplet 1

Zaburi 117:1-2. Enyi mataifa yote, msifuni Bwana, enyi watu wote mhimidi. Maana fadhili zake, kwetu sisi ni kuu, na uaminifu wa Bwana ni wa milele.

Refrain

Zaburi 118: 1-7,2. Mshukuruni Bwana, kwa kuwa ni Mwema. Kwa kuwa fadhili zake ni za milele. Israeli na aseme sasa, ya kwamba fadhili zake, ya kwamba fadhili zake ni za milele.

Couplet 2

Mlango wa Haruni na waseme sasa, ya kwamba fadhili zake ni za milele. Wamchao Bwana na waseme sasa, ya kwamba fadhili zake ni za milele.

Refrain

Zaburi 118: 1-7,2. Mshukuruni Bwana, kwa kuwa ni Mwema. Kwa kuwa fadhili zake ni za milele. Israeli na aseme sasa, ya kwamba fadhili zake, ya kwamba fadhili zake ni za milele.

Couplet 3

Katika shida yangu nalimwita Bwana. Bwana yuko upande wangu, sitaogopa; mwanaDamu atanitenda nini? Bwana yuko upande wangu, msaidizi wangu, msaidizi wangu.