Indirimbo Zikundwa Open in the app

#299

Je, umelisikia jina zuri

Wokovu

Couplet 1

Je, umelisikia jina zuri, Jina la Mwokozi wetu? Linaimbiwa duniani pote na katika watu wote.

Refrain

Yesu, Jina hilo linapita majina yote kwa uzuri! Ni lenye nguvu ya kutuokoa na hatia na makosa.

Couplet 2

Linafariji moyo wa huzuni, latutia raha kuu. Katika shida na hatari huku jina hili latulinda.

Refrain

Yesu, Jina hilo linapita majina yote kwa uzuri! Ni lenye nguvu ya kutuokoa na hatia na makosa.

Couplet 3

Katika giza huku jina hili linang’aa kama nyota, lanipa utulivu na ’hodari siku zote hata kufa.

Refrain

Yesu, Jina hilo linapita majina yote kwa uzuri! Ni lenye nguvu ya kutuokoa na hatia na makosa.

Couplet 4

Majina yote yasahauliwa, ila jina lake Yesu milele litang’aa huko juu. Yesu, jina nzuri mno!