Indirimbo Zikundwa Open in the app

#297

Nipe saa moja nawe Yesu

Wokovu

Couplet 1

Nipe saa moja nawe Yesu nikichoka huku duniani! Hata nikiona vita kali, wanistarehesha siku zote.

Refrain

Nipe saa moja nawe Yesu, kwani giza iko duniani! Natamani kukukaribia, kusikia neno lako zuri.

Couplet 2

Nipe saa moja nawe Yesu katika jaribu na taabu! U makimbilio yangu mema katika hatari na ghasia.

Refrain

Nipe saa moja nawe Yesu, kwani giza iko duniani! Natamani kukukaribia, kusikia neno lako zuri.

Couplet 3

Nipe saa moja nawe Yesu uliechukua dhambi zangu. Ninataka kueleza yote, kwani unanifaamu sana.

Refrain

Nipe saa moja nawe Yesu, kwani giza iko duniani! Natamani kukukaribia, kusikia neno lako zuri.