Indirimbo Zikundwa Open in the app

#296

Dhambi, hatia zimeondolewa

Wokovu

Couplet 1

Dhambi, hatia zimeondolewa, yote ya kale yamepita sasa. Damu ya Yesu imenisafisha; ninamfurahia Mkombozi wangu.

Refrain

Mavazi safi na kao nzuri ninayo huko ju’ Mbinguni. Thawabu nita’pewa huko ni taji ya uzima. Na Yesu ni Mwokozi wangu. Alinikomboa, alilipa deni langu. Pendo lake kubwa nina’sifu siku zote, ninamfurahia Mkombozi.

Couplet 2

Siku za manung’uniko zimekwisha, nimeokoka katika utumwa. Sasa naona raha na furaha sababu Bwana Yesu alinikomboa.

Refrain

Mavazi safi na kao nzuri ninayo huko ju’ Mbinguni. Thawabu nita’pewa huko ni taji ya uzima. Na Yesu ni Mwokozi wangu. Alinikomboa, alilipa deni langu. Pendo lake kubwa nina’sifu siku zote, ninamfurahia Mkombozi.

Couplet 3

Shaka na hofu zimeondolewa, na siogopi kufa kwangu tena. Katika Yesu ninatumaini. Na ninalindwa vema naye siku zote.

Refrain

Mavazi safi na kao nzuri ninayo huko ju’ Mbinguni. Thawabu nita’pewa huko ni taji ya uzima. Na Yesu ni Mwokozi wangu. Alinikomboa, alilipa deni langu. Pendo lake kubwa nina’sifu siku zote, ninamfurahia Mkombozi.

Couplet 4

Roho wa Mungu amenijaliza, anifariji katika mwenendo. Yesu Mwokozi yu karibu nami, aliye ngao yangu na makimbilio.