#292
Katika Damu takatifu ya Mwokozi
Wokovu
Couplet 1
Katika Damu takatifu ya Mwokozi wangu nimesafishwa. Na nguvu ya Mwokozi wangu tu yaweza kunilinda safi.
Refrain
Mungu ahimidiwe, Mungu ashukuriwe kwa ajili ya Wokovu na nguvu ya kushinda! Mungu ahimidiwe, Mungu ashukuriwe kwa ajili ya Wokovu wote!
Couplet 2
Kwa wingi wa Neema yake tu nimeokoka, nimeokoka. Wokovu ni kwa ’jili yako na kwa kila ’aminiye kweli.
Refrain
Mungu ahimidiwe, Mungu ashukuriwe kwa ajili ya Wokovu na nguvu ya kushinda! Mungu ahimidiwe, Mungu ashukuriwe kwa ajili ya Wokovu wote!
Couplet 3
Kwa nguvu zangu sitashinda na siwezi neno, siwezi neno. Ila Yesu anayenifahamu atanisaidia pote.
Refrain
Mungu ahimidiwe, Mungu ashukuriwe kwa ajili ya Wokovu na nguvu ya kushinda! Mungu ahimidiwe, Mungu ashukuriwe kwa ajili ya Wokovu wote!
Couplet 4
Babangu Mwema ananipenda na ananilinda, ananilinda. Sitaogopa giza huku kwa maana yu pamoja nami.