#291
Mimi mwenye hatia nilikombolewa
Wokovu
Couplet 1
Mimi mwenye hatia nilikombolewa, Mwokozi alipojitoa. Dhambi zangu na zako alizichukua, kwa Damu aliniokoa.
Refrain
Dhambi zimetundikwa Msalabani alipojitoa, Mwokozi. Alidharauliwa na kukataliwa atupatanishe na Mungu.
Couplet 2
Yesu mwenye upole na mwenye upendo ananitakasa rohoni. Nimepata uhuru kwa Yesu Mwokozi, alikufa Msalabani.
Refrain
Dhambi zimetundikwa Msalabani alipojitoa, Mwokozi. Alidharauliwa na kukataliwa atupatanishe na Mungu.
Couplet 3
Namwambata Mwokozi, sitaki kumwacha, kwa kuwa alinifilia. Nakusifu, e’ Yesu, unayenipenda, daima nakushangilia.
Refrain
Dhambi zimetundikwa Msalabani alipojitoa, Mwokozi. Alidharauliwa na kukataliwa atupatanishe na Mungu.