#293
Nchi nzuri ya raha ajabu
Wokovu
Couplet 1
Nchi nzuri ya raha ajabu, kwa imani twaona si mbali. Baba atungojea sababu ametuandalia mahali.
Refrain
:/: Tukutane sisi sote huko juu nyumbani mwa Baba!:/:
Couplet 2
Huko juu kwa raha, amani tutaimba na kushangilia, kutolea Mwokozi shukrani kwa sababu alitufilia.
Refrain
:/: Tukutane sisi sote huko juu nyumbani mwa Baba!:/:
Couplet 3
Baba wetu mpendwa na Mwema kwake kuna furaha ya tele. Twamsifu kwa kuwa Neema yatutosha kabisa milele.
Refrain
:/: Tukutane sisi sote huko juu nyumbani mwa Baba!:/: