Indirimbo Zikundwa Open in the app

#290

Baragumu litalia sana

Wokovu

Couplet 1

Baragumu litalia sana, watu Wake watalisikia. Waliokufa watafufuka na wazima watabadilika. :/: Nani Anayeweza? Yesu, Mweza yote. :/:

Couplet 2

Na wenye uwezo wa dunia watatetemeka siku ile, na hawataweza kuinuka kutazama uso kama jua. :/: Nani Anayeweza? Yesu, Mweza yote. :/:

Couplet 3

Najua Mchunga wangu Mwema, anichunga kwa maisha yangu. Na siku ya mwisho nikishinda, sitaona uchungu wa kufa. :/:Nani Mchunga Mwema? Yesu, Mweza yote. :/:

Couplet 4

Mbinguni hakitafika kitu cha uchafu, dhambi na kuasi. Wasiomwamini Bwana Yesu, gadhabu ya Mungu yawangoja. :/: Nani Atahukumu? Yesu, Mweza yote. :/:

Couplet 5

Mimi Yesu mzabibu kweli, Baba Mungu ndiye mkulima, na ninyi matawi ndani yangu, na hamwezi neno bila mimi. :/: Nani ni Mzabibu? Yesu, Mweza yote. :/:

Couplet 6

Unayempenda Baba Mungu, lazima upende ndugu yako; ukiwa hupendi ndugu yako, huwezi kupenda Baba Mungu. :/:Nani Aliyesema? Yesu, Mweza yote. :/:

Couplet 7

Nawapenda, mwisho wa upendo, na ninyi mpate kupendana; hivyo mataifa wataona ya kwamba m watu wangu kweli. :/: Nani Mwenye Upendo? Yesu, Mweza yote. :/:

Couplet 8

Sisi watumishi wake Mungu, tumeacha vyote vya dunia. Tumemchagua Bwana Yesu, tuwekwe kuume kwake Mungu. :/: Tumshukuru nani? Yesu Mweza yote. :/: