Indirimbo Zikundwa Open in the app

#289

Ninatamani kwenda Mbingu

Wokovu

Couplet 1

Ninatamani kwenda Mbingu nchi yangu niliyopewa na Mungu kwa imani. Ni shangwe bora kuona mji ule; kwa kwenda kule sitaogopa kitu.

Refrain

E’ Baba yangu, niongoze, unisafishe kwa Damu ya Mwokozi! Nifananishwe na theluji, unibatize kwa Roho ’takatifu!

Couplet 2

E’ Mungu, tumepata Mwana Yesu Kristo, kipawa kweli kinachoshinda yote. Anahubiri amani kwao wote walio huku karibu, nao mbali.

Refrain

E’ Baba yangu, niongoze, unisafishe kwa Damu ya Mwokozi! Nifananishwe na theluji, unibatize kwa Roho ’takatifu!

Couplet 3

Kwa Yesu tumepata mwisho wa upendo na njia ya kumwendea Baba Mungu. Si wapitaji na tena si wageni, tunatumika kwa roho ya upendo.

Refrain

E’ Baba yangu, niongoze, unisafishe kwa Damu ya Mwokozi! Nifananishwe na theluji, unibatize kwa Roho ’takatifu!

Couplet 4

Amani kwetu na matumaini tele, salamu toka kwa Mungu wa milele ni posho ya watumishi wa upendo; tunaurithi uzima wa milele.

Refrain

E’ Baba yangu, niongoze, unisafishe kwa Damu ya Mwokozi! Nifananishwe na theluji, unibatize kwa Roho ’takatifu!