Indirimbo Zikundwa Open in the app

#286

Yesu, ulikaribishwa arusini

Wokovu

Couplet 1

Yesu, ulikaribishwa arusini huko Kana; hapo ikadhihirishwa nguvu yako kwa ishara.

Couplet 2

Leo tunakuhitaji, wabariki ndugu hawa: Bwana na bibi-arusi! Ndoa yao iwe sawa!

Couplet 3

Katika taabu, raha, wafungane kwa upendo! Watumike kwa furaha, w’andamane kati’ mwendo!

Couplet 4

Yesu, U mlinzi wao, uwalinde na mabaya! Uhifadhi nyumba yao! Tunaomba mema haya!