Indirimbo Zikundwa Open in the app

#287

Tunamtia mikononi mwako mtoto

Wokovu

Couplet 1

Tunamtia mikononi mwako mtoto huyu, umtunze sana, na kila siku kwa Neema yako umbariki, Bwana Yesu Kristo!

Couplet 2

Ulimwengu kuna majaribu mahali pote, shida na mitego. Lakini uwe mchungaji wake, na umwongoze, E’ rafiki Mwema!

Couplet 3

Mwokozi kwa upendo ’mchukue, asije akashindwa safarini! Na umlinde kwa rehema yako, apate kuwa wako siku zote!

Couplet 4

Utume nuru ya Neema kwake na maji ya uzima toka kwako e Bwana Yesu. Twakuomba leo ulinde mwana wetu kwa salama.