#285
Neno la Mungu ndani ya Biblia
Wokovu
Couplet 1
Neno la Mungu ndani ya Biblia limetolewa na Mwenyezi Mungu. Biblia yetu inatuambia: Njoo kwa Yesu, Mkombozi wetu!
Refrain
Neno la Mungu tulilolipewa, njia ya Mbingu limetuonyesha; nuru gizani ya kutuongoza katika mwendo wetu kwenda Mbinguni.
Couplet 2
Siku za giza zinakaribia, kama walivyosema manabii. Biblia yetu itatuangaza na kutuonya njia hata mwisho.
Refrain
Neno la Mungu tulilolipewa, njia ya Mbingu limetuonyesha; nuru gizani ya kutuongoza katika mwendo wetu kwenda Mbinguni.
Couplet 3
Katika neno la Biblia yetu tunaupata utajiri wote. Mbingu na nchi zitaangamia, neno la Mungu litashinda yote.