Indirimbo Zikundwa Open in the app

#284

Usimtafute Yesu kati’ wafu

Wokovu

Couplet 1

Usimtafute Yesu kati’ wafu kaburini! Yu mzima, tumsifu, hakushindwa na kuzimu! :/: Yesu hai, Yesu hai, mshindaji wa mauti! :/:

Couplet 2

Maadui walifunga Bwana Yesu kaburini, Mungu alimfufua Mwana wake. Furahini! :/: Yesu hai, Yesu hai, imba hivyo duniani! :/:

Couplet 3

Yesu hai, ni habari ya kupasha pande zote. Yu Mwokozi wetu kweli, alitufilia sote. :/: Yesu hai, Yesu hai, Mkombozi asifiwe!:/: