Indirimbo Zikundwa Open in the app

#281

Yote ninayo niliyapokea kwa wema

Wokovu

Couplet 1

Yote ninayo niliyapokea kwa wema wake unaonea. Namsifu Yesu, namtegemea, aliniokoa kwa neema.

Refrain

Niliyekuwa nimetoroka, kwa pendo lake nimeokoka. Yesu yu Mwema na mwenye rehema, nimeokolewa kwa neema!

Couplet 2

Nilitembea zamani dhambini katika njia ya kufa, lakini Yesu alinitafuta porini, akaniokoa kwa neema.

Refrain

Niliyekuwa nimetoroka, kwa pendo lake nimeokoka. Yesu yu Mwema na mwenye rehema, nimeokolewa kwa neema!

Couplet 3

Natakasiwa na Yesu Mwokozi, si kwa majuto na si kwa machozi, bali kwa Damu, ninao ’kombozi; nimeokolewa kwa neema.

Refrain

Niliyekuwa nimetoroka, kwa pendo lake nimeokoka. Yesu yu Mwema na mwenye rehema, nimeokolewa kwa neema!

Couplet 4

Raha ya Mbingu imeniingia, kwa shangwe kubwa ninafurahia Yesu, kwa kuwa anirehemia; nimeokolewa kwa neema.