Indirimbo Zikundwa Open in the app

#282

Ukiona kiu sana ujalivu wa Mwokozi

Wokovu

Couplet 1

Ukiona kiu sana ujalivu wa Mwokozi, roho yake safi pia, liamini neno la babako na atakujazi, nawe utashangilia.

Refrain

Atakujaliza hata utashiba. Bwana Yesu akuita: "Njoo bila ’sitasita!" Atakujaliza hata utashiba Roho na uwezo wake.

Couplet 2

Vichukue vyombo vyako, uvioshe safi sana kisimani pa Golgotha! Afadhali kujitoa lote kwa Mungu Bwana, na imani itaota.

Refrain

Atakujaliza hata utashiba. Bwana Yesu akuita: "Njoo bila ’sitasita!" Atakujaliza hata utashiba Roho na uwezo wake.

Couplet 3

Na mafuta ya Neema hayakomi. Asifiwe! Tunakuwa na shukrani! Anataka kumimina Roho ya ahadi yake. Mpokee kwa imani!

Refrain

Atakujaliza hata utashiba. Bwana Yesu akuita: "Njoo bila ’sitasita!" Atakujaliza hata utashiba Roho na uwezo wake.