#280
Jina lake Yesu Kristo linadumu
Wokovu
Couplet 1
Jina lake Yesu Kristo linadumu siku zote; jina hili la milele haliwezi kunyauka; linafaa watu wote, na wazee na vijana; linaweza kuongoza kila mtu kwake Mungu.
Refrain
Jina hili nalipenda, limewasha moyo wangu; na kwa jina hili jema nimepata kuokoka.
Couplet 2
Jina hili linavuma pande zote za dunia, na kwa wote linaleta tumaini na faraja. Jina hili laondoa uadui na ubaya, hata milki ya Mwokozi itaanza kutawala.
Refrain
Jina hili nalipenda, limewasha moyo wangu; na kwa jina hili jema nimepata kuokoka.
Couplet 3
Na katika giza huku jina hili linang’aa, laonyesha msafiri njia wazi ya uzima. Jua likitiwa giza, jina hili linadumu; na milele lisifiwe hapa na Mbinguni juu.
Refrain
Jina hili nalipenda, limewasha moyo wangu; na kwa jina hili jema nimepata kuokoka.