#278
Ninainua macho yangu kwa Mungu
Wokovu
Couplet 1
Ninainua macho yangu kwa Mungu aketiye juu, aliye msaada wangu, njiani pangu nuru kuu. Aliyefanya yote, maombi huyasikia. Katika njia zangu zote atanilinda pote pia.
Couplet 2
Bwanangu asiache tena mguu wangu usogezwe, kwa kuwa ni mlinzi Mwema, naye hatasinzia kamwe. Alinda roho yangu nisije nikapotea. Hitaji za maisha yangu baraka yake ya’enea.
Couplet 3
Aniokoa na uovu, na roho yangu imepona. Kwa yeye nguvu na Wokovu, nilizionja naku’ona. Ananilinda pote: kutoka na kuingia; anijaliza mema yote hata nakutumainia.