Indirimbo Zikundwa Open in the app

#277

Nitaogopa nini gizani duniani?

Wokovu

Couplet 1

Nitaogopa nini gizani duniani? Sikuachiwa peke’ mbali ya tumaini! Mwokozi yu karibu, asiyebadilika. :/: Hutunza ndege ndogo na mimi kadhalika:/:

Refrain

Namshukuru Mungu asiyebadilika. Hutunza ndege ndogo na mimi kadhalika.

Couplet 2

"E’ usifadhaike moyoni mwako, mwana", anong’oneza Yesu, "Nitegemee sana!" Na hapo woga wangu waruka kwa hakika. :/: Hutunza ndege ndogo na mimi kadhalika:/:

Refrain

Namshukuru Mungu asiyebadilika. Hutunza ndege ndogo na mimi kadhalika.

Couplet 3

Na nikijaribiwa na jua lifichwapo, hata sioni raha, wala faraja hapo, nakimbilia Yesu, na yote yapinduka. :/: Hutunza ndege ndogo na mimi kadhalika:/:

Refrain

Namshukuru Mungu asiyebadilika. Hutunza ndege ndogo na mimi kadhalika.