Indirimbo Zikundwa Open in the app

#276

Matendo ya Mungu yapita fahamu

Wokovu

Couplet 1

Matendo ya Mungu yapita ’fahamu, ni nani ayaona wazi? Lakini najua mapito ya Mungu kwa mimi yafaa halisi.

Couplet 2

Njiani sijui maana ya yote, lakini nitayafaamu. Kwa nini kuzisumbukia kwa bure taabu na shida za mda?

Couplet 3

E’ Bwana, unayo magari maelfu, na lenye linalonifaa, u’lichagulie mwenyewe, Bwanangu, nifike salama Mbinguni!

Couplet 4

Na kama Elia upesi kabisa nitakavyoacha dunia, uchungu na shida za huku ’takwisha, milele nitashangilia.

Couplet 5

Tutamsujudu Mwokozi daima, kuimba maelfu pamoja: E’ Mungu, u haki na mwenye Neema katika shauri na tendo.

Couplet 6

Halafu nangoja kwa uvumilivu kujua maana kwa wazi. Na matumaini ni yenye uzima: Urithi ninao Mbinguni.