Indirimbo Zikundwa Open in the app

#275

E’ Mungu mwenye haki uniongoze

Wokovu

Couplet 1

E’ Mungu mwenye haki, uniongoze huku katika mambo yote yanayokupendeza! Nikiwa huku bila wewe, vitisho hofu na mashaka yananitia tetemeko mpaka kufa.

Couplet 2

Ni heri siku zote kutegemea Yesu na kuenenda sawa katika nyayo zake, kwa kuwa yeye ni Mchunga anayeniongoza vema, nipate kuingia katika raha yake.

Couplet 3

Safari yangu sasa yaelekea Mbingu, Mwokozi yuko huko, lazima nifikeko na siku nitakapofika ’tashangilia kwa furaha kuona yeye aliyeninunua kwake.

Couplet 4

Ulimwenguni humu, matata na kuchoka. Nikihitaji kitu nafadhahika bure, lakini siku ile kuu nita’pomwona Mkombozi, natumaini sitakosa dhawabu yangu!

Couplet 5

Mbinguni sitaona adui zangu tena. Hayatakuwa mambo yakupokonya pale. Sauti nitamtolea, kusema: Mungu, haleluya! Mikono nitaipepea kwa shangwe kuu!