#274
Ninafurahia kisima daima
Wokovu
Couplet 1
Ninafurahia kisima daima, kisima cha Damu ya Yesu. Katika upendo nalindwa salama, nasifu Mwokozi mpendwa.
Refrain
Kisima cha maji kinabubujika, kinaniletea uzima. Na kando ya maji ninaburudika, ninashangilia daima.
Couplet 2
Nakaa karibu ya kisima hiki, naishi kwa maji ya ’hai. Yananilietea kupita kipimo uzima na shangwe rohoni.
Refrain
Kisima cha maji kinabubujika, kinaniletea uzima. Na kando ya maji ninaburudika, ninashangilia daima.
Couplet 3
Nakaa karibu ya kisima hiki, naishi katika uheri. Ufike upesi ulie na kiu, kisima kinabubujika!
Refrain
Kisima cha maji kinabubujika, kinaniletea uzima. Na kando ya maji ninaburudika, ninashangilia daima.
Couplet 4
Nakaa karibu ya kisima hiki, naona furaha na raha. Nakando ya maji nafasi kwa wote, waweza kupona kabisa.