Indirimbo Zikundwa Open in the app

#268

E’ Yesu, ingia rohoni kabisa

Wokovu

Couplet 1

E’ Yesu, ingia rohoni kabisa, uniweke huru nakunitakasa, nipate kushirikiana na wewe katika mateso na raha daima!

Refrain

:/: E’ Bwana, nijaze upendo wa Mbingu nao uthabiti, niwe mshindaji! :/:

Couplet 2

Siombi ufalme, siombi heshima, naomba kupewa Neema daima, nijue ukweli wa neno la Mungu: Mtoe miili na iwe dhabihu!

Refrain

:/: E’ Bwana, nijaze upendo wa Mbingu nao uthabiti, niwe mshindaji! :/:

Couplet 3

Ingia rohoni, unichungulie, na katika yote unisaidie, nipate kabisa kusudi na nia kujitoa kwako, kukutumikia!

Refrain

:/: E’ Bwana, nijaze upendo wa Mbingu nao uthabiti, niwe mshindaji! :/:

Couplet 4

Hakuna la huku litanizuia nisifananishwe na Yesu Masiya. Nitumainije kufika Mbinguni nisiposhiriki Mwokozi mpendwa!

Refrain

:/: E’ Bwana, nijaze upendo wa Mbingu nao uthabiti, niwe mshindaji! :/: