Indirimbo Zikundwa Open in the app

#267

Baba nakuomba leo na mapema

Wokovu

Couplet 1

Baba, nakuomba leo na mapema: Niongoze pote kwa mapito mema!

Refrain

Baba yangu, sikiliza ombi langu leo! Baba, nakusifu! Unanisikia.

Couplet 2

Nistahimilipo kazi za mchana, unitie nguvu, nakuomba, Bwana!

Refrain

Baba yangu, sikiliza ombi langu leo! Baba, nakusifu! Unanisikia.

Couplet 3

Hata jua kuchwa liagapo njia, Baba, nakuomba: Unilinde pia!

Refrain

Baba yangu, sikiliza ombi langu leo! Baba, nakusifu! Unanisikia.

Couplet 4

Maadui wengi watuwindawinda, kwa maisha yetu Mungu ni mlinda.

Refrain

Baba yangu, sikiliza ombi langu leo! Baba, nakusifu! Unanisikia.

Couplet 5

Katika utoto na ujana tena, na uzee pia: omba, kesha, shinda!