Indirimbo Zikundwa Open in the app

#266

Ayala naye anayo shauku ya maji

Wokovu

Couplet 1

Ayala naye anayo shauku ya maji ya kisima; na vivyo hivyo ninaona kiu kwa Mungu wa uzima.

Refrain

Kama ayala aonavyo shauku mito ya maji safi, na vivyo hivyo rohoni mwangu naona kiu kwa Mungu wangu.

Couplet 2

E’ Mungu wangu, Mungu wa fadhili, nakutafuta wewe! Je, nikuone lini kwa ’kamili, niburudishwe nawe!

Refrain

Kama ayala aonavyo shauku mito ya maji safi, na vivyo hivyo rohoni mwangu naona kiu kwa Mungu wangu.

Couplet 3

Nazifikiri siku za zamani niliposhangilia. Nijaze tena raha na amani, nakutumainia!

Refrain

Kama ayala aonavyo shauku mito ya maji safi, na vivyo hivyo rohoni mwangu naona kiu kwa Mungu wangu.

Couplet 4

Na usifadhaike moyo wangu, amini Mungu wako! Fadhili zake hata huko Mbingu zatosha sana kwako!