#265
Tu wasafiri, twakaribia nchi
Wokovu
Couplet 1
Tu wasafiri, twakaribia nchi ya Mbingu kwa Mungu baba. Tusiogope bonde la kufa, Yesu atuongoza kwake!
Refrain
:/: Tu wasafiri:/: tutakutana nyumbani mwa Baba. E’ Bwana Yesu utuongoze, tufike sote Mbinguni!
Couplet 2
Wengi katika wapendwa wetu wamevuka mto wa kufa. Walifuata mwito wa Mungu. Wakahamia nchi nzuri.
Refrain
:/: Tu wasafiri:/: tutakutana nyumbani mwa Baba. E’ Bwana Yesu utuongoze, tufike sote Mbinguni!
Couplet 3
Katika mwendo wa duniani walitazama Mwokozi wao, na waliacha mambo ya huku, walipendeza Bwana Yesu.
Refrain
:/: Tu wasafiri:/: tutakutana nyumbani mwa Baba. E’ Bwana Yesu utuongoze, tufike sote Mbinguni!
Couplet 4
Ndugu wapendwa, tuendelee, hata ikiwa shida njiani! Yesu ni njia, kweli, uzima; tumfuate siku zote!