Indirimbo Zikundwa Open in the app

#264

E’ msafiri jangwani, tazama juu

Wokovu

Couplet 1

E’ msafiri jangwani, tazama juu Mbinguni! Hapo utaona nyota za faraja na tumaini.

Refrain

Huko hutayaona machozi wala shida. Mungu atatuliza msafiri Mbinguni kwake.

Couplet 2

Ukisumbuka gizani katika pepo, dhoruba, bado wakati mfupi, nuru itatokea tena.

Refrain

Huko hutayaona machozi wala shida. Mungu atatuliza msafiri Mbinguni kwake.

Couplet 3

Ukililia wapendwa waliokutangulia, utakutana na wote, hutalia machozi tena.

Refrain

Huko hutayaona machozi wala shida. Mungu atatuliza msafiri Mbinguni kwake.

Couplet 4

Na karibu na Bwana Yesu utastarehe daima, hutakumbuka Mbinguni shida, kufa na sikitiko.

Refrain

Huko hutayaona machozi wala shida. Mungu atatuliza msafiri Mbinguni kwake.