Indirimbo Zikundwa Open in the app

#263

Enyi kundi lake Mungu

Wokovu

Couplet 1

Enyi kundi lake Mungu, muda haba mhimili! Kati’ nchi ya milele mtaona raha tele. :/: Muda haba, muda haba, tena vita itakwisha. :/:

Couplet 2

Usilogwe na dunia, usiache Mungu wako! Katika mabaya, mema ufuate Bwana Yesu. :/: Siku zote, siku zote! Hivyo utashinda vyote. :/:

Couplet 3

Ukichoka safarini, ukiona njia ndefu na hatari za jangwani, Mungu akuburudisha. :/: Raha huko, raha huko yatuliza msafiri. :/:

Couplet 4

Kwa imani tunaona nchi yetu ya ahadi. Ni habari nzuri sana: Majaribu yatakoma. :/: Mbio sana, mbio sana huko ju’ tutaonana. :/:

Couplet 5

Tukiitwa na mauti kwa furaha tutahama. Tulivyovitumaini, ng’ambo huko tutaona. :/: Heri tele, heri tele: ’ona raha ya milele! :/: