Indirimbo Zikundwa Open in the app

#262

Kitambo bado- vita itaisha

Wokovu

Couplet 1

Kitambo bado-vita itaisha, kitambo, na dhoruba zitapoa. Na tena nitalaza kichwa changu mbavuni mwake anayenipenda. :/: Nitaziona raha na amani, Mbinguni hazitakuwapo dhambi. :/:

Couplet 2

Kitambo bado- roho yaumizwa, kitambo katika usiku huku. Machozi nina’toka mara nyingi sababu sijaona bado Yesu. :/: Lakini asubuhi ya milele huko Mbinguni sitalia tena. :/:

Couplet 3

Kitambo bado ya kuchoka huku, kitambo, tena nitaona Yesu. Na huru mbali na hatari zote nitastarehe mikononi mwake. :/: Uvuli wote utaondolewa kwa nuru huko kamilifu kweli. :/:

Couplet 4

Mateso yangu hayadhuru tena, nitasahau yote kwa Yesu. Nikisumbuka mda duniani, Mbinguni sitaona shida, kufa. :/: Na Mungu atafuta kila chozi, ataondoa maumivu yote. :/: