#261
Msafiri ulie njiani
Wokovu
Couplet 1
Msafiri uliye njiani, watamani nyumba ya babako. Sikiliza nyimbo za Mbinguni! U karibu sana kufikako.
Refrain
Utakuwako huko, katika mkutano wa Wakristo huko Mbinguni kwa raha ipitayo fahamu? Utakuako huko wakati wa kuimba wimbo mpya wa kumsifu Mwokozi siku zote?
Couplet 2
Sikiliza sasa makengele yapigwayo huko juu kwetu, ili kutuita sisi mbele ya jioni ya maisha yetu!
Refrain
Utakuwako huko, katika mkutano wa Wakristo huko Mbinguni kwa raha ipitayo fahamu? Utakuako huko wakati wa kuimba wimbo mpya wa kumsifu Mwokozi siku zote?
Couplet 3
Labda siku ile ni karibu nitakapokwenda, nitahama! Sitaona tena majaribu, nitajazwa kwa kumtazama.
Refrain
Utakuwako huko, katika mkutano wa Wakristo huko Mbinguni kwa raha ipitayo fahamu? Utakuako huko wakati wa kuimba wimbo mpya wa kumsifu Mwokozi siku zote?
Couplet 4
Lango la Mbinguni wazi sasa, Yesu amelifungua kwako. Utaweza kuokoka hasa, usiharibishe heri yako!