Indirimbo Zikundwa Open in the app

#258

Mkutano ’kubwa gani mlimani

Wokovu

Couplet 1

Mkutano ’kubwa gani mlimani mwa Sayuni asubuhi ya milele? Hawa walinunuliwa tena walitakasiwa, wawe malimbuko kwa Mwokozi.

Couplet 2

Hata kufa huku chini walikuwa waamini, walimfuata Yesu. Sasa wanaka’ Mbinguni, wametoka jaribuni, wamerithi raha yakipeo.

Couplet 3

Ukamili wa uzuri wa muziki na zaburi unatoka huko juu! Ni sauti tamu mno ya kinubi na ya wimbo kandokando ya Mwokozi wetu!

Couplet 4

Wimbo huo ni wa nani, wa sauti ya tufani, wa kutia raha kuu? Ndio wimbo mpya ule uimbwao sasa kule ili kuhimidi Mkombozi.

Couplet 5

Bwana, unilinganishe, na ulimi u’safishe, nami nikaimbe huko! Nipe vazi la rohoni, safi sana, la kitani lifaalo asubuhi hiyo!