Indirimbo Zikundwa Open in the app

#259

Nafikiri siku tutakayofika Mbinguni

Wokovu

Couplet 1

Nafikiri siku tutakayofika Mbinguni huko kwetu, na malaika kwa furaha watatukaribisha.

Refrain

Wataimba wimbo wakutupokea: "Karibuni! Karibuni wote kwetu!" Malaika wa Mungu watatulaki kwa nyimbo za furaha: "Twawasalimu! Karibu kwetu!"

Couplet 2

Mkutano ’kubwa umekwenda mbele na sasa uko kule. Huimba kwa sauti kuu ukimsifu Mungu.

Refrain

Wataimba wimbo wakutupokea: "Karibuni! Karibuni wote kwetu!" Malaika wa Mungu watatulaki kwa nyimbo za furaha: "Twawasalimu! Karibu kwetu!"

Couplet 3

Sisi nasi tutakusanyika huko Yerusalemu mpya, na mkutano wa Wakristo utatuamkia.

Refrain

Wataimba wimbo wakutupokea: "Karibuni! Karibuni wote kwetu!" Malaika wa Mungu watatulaki kwa nyimbo za furaha: "Twawasalimu! Karibu kwetu!"

Couplet 4

Bwana Yesu naye atatupokea, atatukumbatia katika nyumba ya Mbinguni iliyo ya milele.