Indirimbo Zikundwa Open in the app

#257

Siku ya kuisikia parapanda

Wokovu

Couplet 1

Siku ya kuisikia parapanda yake Mungu, ikiita wateule wake wote, kwa Neema tutakaribishwa na Mwokozi wetu katika kutano kubwa huko juu.

Refrain

Tutakaribishwa kwake, tutakaribishwa kwake, tutakaribishwa kwake katika kutano kubwa huko juu.

Couplet 2

Mungu anawafufua wafu wake siku ile, na Wakristo hai watabadilika, wote watanyakuliwa kumkuta Bwana Yesu, tutakusanyika wote huko juu!

Refrain

Tutakaribishwa kwake, tutakaribishwa kwake, tutakaribishwa kwake katika kutano kubwa huko juu.

Couplet 3

Wimbo wa Mbinguni kama maji utakapovuma, utukufu wake Yesu tuta’ona. Nami pia kwa Neema nitafika siku ile kusikia neno lake la "karibu!"

Refrain

Tutakaribishwa kwake, tutakaribishwa kwake, tutakaribishwa kwake katika kutano kubwa huko juu.