Indirimbo Zikundwa Open in the app

#256

Asubuhi na mapema siku ya habari

Wokovu

Couplet 1

Asubuhi na mapema siku ya habari njema twende sote Bethlehemu! Mungu ameturehemu!

Couplet 2

Nyota kubwa inang’aa ju’ ya nyumba ana’kaa Mwana wake wa pekee. Mbele yake tujiweke!

Couplet 3

Wachungaji wasikia nyimbo zao malaika: " Asifiwe Mungu juu, duniani raha kuu!"

Couplet 4

Mariamu anachoka, safarini wana’toka, analaza mwana ndani ya sanduku la majani.

Couplet 5

Wachungaji wanafika, na magoti wana’piga; waliacha kundi lote kushukuru Yesu wote.

Couplet 6

Mwana yule ni Mwokozi, msaada, Mkombozi. Neno la kuaminiwa, Mungu ametushukia!