Indirimbo Zikundwa Open in the app

#249

Zamani mjini mwa Yerusalemu

Wokovu

Couplet 1

Zamani mjini mwa Yerusalemu waisrael’ waliabudu. Wakristo wa sasa wanakusanyika kuomba, kusifu Mwokozi.

Refrain

Msifuni, msifuni Mungu wetu, kwani ametutendea mema! Tutamsifu tu aliyetoka ju’, shangilieni Mwokozi Mwema!

Couplet 2

Mwokozi yu nasi, ame’fumbulia uweza wa kutuokoa. Na yu mwaminifu, atusikiliza, apenda kutupa baraka.

Refrain

Msifuni, msifuni Mungu wetu, kwani ametutendea mema! Tutamsifu tu aliyetoka ju’, shangilieni Mwokozi Mwema!

Couplet 3

Twaomba baraka na mvua ya Mbingu kuithibitisha Injili! Wagonjwa wapone, vipofu waone, Tupate ’batizo wa Roho!

Refrain

Msifuni, msifuni Mungu wetu, kwani ametutendea mema! Tutamsifu tu aliyetoka ju’, shangilieni Mwokozi Mwema!