Indirimbo Zikundwa Open in the app

#247

Napenda sana kumshukuru Mwokozi

Wokovu

Couplet 1

Napenda sana kumshukuru Mwokozi wangu kwa nia huru; kwa wimbo wangu nashuhudia upedo wake na Damu pia.

Couplet 2

Nikishukuru mateso yake Msalabani na kufa kwake, nataka katika wimbo wangu kumtolea shukrani yangu.

Couplet 3

Naimba sasa, nina faraja, katika Yesu nina faraja. Ni mambo tunayofunuliwa, kwa wenye dhambi yamefichwa.

Couplet 4

Kwa neno lake ananiambia kwamba ananihurumia, na ukombozi ninao sasa kwa Damu iliyonitakasa.

Couplet 5

Na msione ajabu sana ya kuwa namshukuru Bwana! Ninamwimbia kidogo sasa, ’taendelea Mbinguni hasa.

Couplet 6

Anipa vyote kwa pendo lake, urithi wangu wachungwa kwake hata wakati wakuhamia Mbinguni, na nitashangilia.