#238
Nifananishwe nawe Mwokozi
Wokovu
Couplet 1
Nifananishwe nawe Mwokozi, ni haja yangu iliyo kuu. Ninakuomba, na kwa machozi, nikufuate, Bwana wa juu!
Refrain
Nifananishwe nawe Mwokozi, mwenye Upendo, safi halisi! Unitakase, Unijalize! Nifananishwe nawe zaidi!
Couplet 2
Nifananishwe nawe Mwokozi, mwenye Rehema, Pendo ajabu! Niwapeleke kwa Mkombozi walioshindwa na majaribu!
Refrain
Nifananishwe nawe Mwokozi, mwenye Upendo, safi halisi! Unitakase, Unijalize! Nifananishwe nawe zaidi!
Couplet 3
Nifananishwe nawe Bwanangu, Mtakatifu, mwenye saburi! Niwe mnyofu kazini mwangu, mtu thabiti bila jeuri!
Refrain
Nifananishwe nawe Mwokozi, mwenye Upendo, safi halisi! Unitakase, Unijalize! Nifananishwe nawe zaidi!
Couplet 4
Nifananishwe nawe Mwokozi! Ninakuomba: Unijarize! Vyote ninavyo nakutolea, Uniongoze, Uniagize!
Couplet 5
Nifananishwe nawe Mwokozi! Nimiminie pendo moyoni! Nibadilishe, e’ Mkombozi, niwe tayari kwenda Mbinguni!
Refrain
Nifananishwe nawe Mwokozi, mwenye Upendo, safi halisi! Unitakase, Unijalize! Nifananishwe nawe zaidi!