Indirimbo Zikundwa Open in the app

#239

Neno baya lisitoke kamwe...

Wokovu

Couplet 1

Neno baya lisitoke kamwe kwa ulimi wako! Pendo likuchunge pote, hata na maneno yako!

Refrain

Amri ya Yesu ni "Mpendane"! Kama watoto wema tumtii! Amri ya Yesu ni "Mpendane"! Kama watoto tumtii!

Couplet 2

Pendo ni la Mbingu, safi, urafiki ’takatifu. Tusiyaharibu tena kwa maneno yetu ’gumu!

Refrain

Amri ya Yesu ni "Mpendane"! Kama watoto wema tumtii! Amri ya Yesu ni "Mpendane"! Kama watoto tumtii!

Couplet 3

Neno moja la hasira au tendo la uovu, kwa upesi linavunja fungu la upendo safi.

Refrain

Amri ya Yesu ni "Mpendane"! Kama watoto wema tumtii! Amri ya Yesu ni "Mpendane"! Kama watoto tumtii!