Indirimbo Zikundwa Open in the app

#237

Mwokozi wangu ni Mwamba bora

Wokovu

Couplet 1

Mwokozi wangu ni Mwamba bora, ahadi kama milima; zaniletea amani tele, na mibaraka daima. Katika Mwamba ni raha kuu, baraka tele kutoka juu. Nakaa humo, ninastarehe, ni heri sana milele.

Couplet 2

Makimbilio ni Mwamba huo katika teso lo lote; Nisikimbie adui ’kuu, nishinde katika vyote! Dunia yote ikitingika, ahadi zake hazipunguki. Nakaa humo, ninastarehe, ni heri sana milele.

Couplet 3

Nakaa mbali ya udhalimu, hatia, dhambi, hukumu. Na kwa imani nikisimama, adui atakimbia. Nayo mawazo ya giza tupu hayatapata nafasi huko. Nakaa humo, ninastarehe, ni heri sana milele.

Couplet 4

Nafurahia baraka zote za ulimwengu wa roho. Karama hizo nilizipewa katika kufa kwa Yesu. Hakuna woga na shaka huko, hayatakuwa manung’uniko. Nakaa humo, ninastarehe, ni heri sana milele.