#234
Utukufu wa Mbinguni ni wa heri
Wokovu
Couplet 1
Utukufu wa Mbinguni ni wa heri na amani, dhambi hazitakuwamo. Vitu vyote vilivyomo ni vya tunu na thamani, dhambi hazitakuwamo.
Refrain
Dhambi hazitaingia Mbingu ya utakatifu. Ukidumu mwenye dhambi bila kutakaswa huku, hutaingia Mbinguni.
Couplet 2
Kama unatumaini kufikia nchi ile na kuona Bwana Yesu, utafute utakaso na kupata moyo safi! Dhambi hazitakuwamo.
Refrain
Dhambi hazitaingia Mbingu ya utakatifu. Ukidumu mwenye dhambi bila kutakaswa huku, hutaingia Mbinguni.
Couplet 3
Unaweza ’tenda dhambi na kukana Bwana Yesu, walakini ukumbuke: Dhambi zako zitafunga lango la Mbinguni, kwani dhambi hazitakuwamo.
Refrain
Dhambi hazitaingia Mbingu ya utakatifu. Ukidumu mwenye dhambi bila kutakaswa huku, hutaingia Mbinguni.
Couplet 4
Na ukiwa mkaidi hata sa’ ya kufa kwako, utaitwa hukumuni, na utaambiwa huko: "Ondokeni siwajui!" Dhambi hazitakuwamo.
Refrain
Ukitaka kufikako Mbingu ya utakatifu, tubu sasa, hacha dhambi, utafute moyo safi, na utaingia Mbingu!